Feitoto achekelea ujio wa Ibenge, Azam FC


"Msimu ujao utakuwa Mzuri Mimi kama mchezaji nimejiandaa, ila mambo ya msimu ujao nisingependa kuyazungumza kawaulize uongozi wa Azam FC

Ujio wa Ibenge Mimi kama mchezaji nimefurahi, ni Kocha mwenye Cv kubwa tutafanya kazi maisha mengine yanaendelee"

Feisal Salum akizungumza kuhusu ujio wa kocha Mpya wa Azam FC Florent Ibenge, Fei ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya kutamatika kwa tamasha la Wape Tabasamu.