ES Setif yamtambulisha kiungo wa Yanga

ALIYEKUWA winga wa Azam FC ya Dar es Salaam, Gibril Sillah raia wa Gambia amejiunga na ES Setif ya Algeria.

Setif ilipost jana kumtambulisha na kumkaribisha mchezaji huyo aliyeondoka Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake.

Sillah aliwasili Azam FC katika dirisha dogo Januari 7, mwaka 2023 akitokea Raja Casablanca ya Morocco baada ya awali kuchezea timu nyingine nchini humo, JS Soualem.

Alijiunga na Raja Agosti 27 mwaka 2021 akitokea Teungueth ya Senegal, lakini Januari 24 mwaka 2022 akapelekwa kwa mkopo JS Soualem alikocheza hadi anasajiliwa Azam FC.

Kabla ya kwenda Teungueth Julai 1, mwaka 2017 alichezea Samger FC na Fortune FC za kwao, Gambia.