Denis Nkane kutimkia Kagera Sugar kwa mkopo

Uongozi wa Kagera Sugar upo katika mazungumzo ya kupata saini ya nyota wa Yanga, Denis Nkane kwa mkopo wakiwa na imani anaweza kukisaidia kikosi cha timu hiyo.

"Tunasubiri ma jibu kutoka Yanga, lakini hiyo ofa tayari tumeshaituma na tunaaamini kama tutampata mchezaji huyo ataongeza kitu ndani ya timu yetu hivyo dirisha hili tunahitaji kujiimarisha," kilisema chanzo.