Mwenyekiti wa Klabu ya Al-Hilal, Hisham Hassan Al-Subat leo Amekutana na Kocha Florent Ibenge katika Ofisi zake zilizopo Huko Port, Sudan Kwa ajili ya kumuaga na kumtakia kila la heri kwa maisha yake nje ya Al Hilal.
Ibenge tayari amemalizana na Al Hilal na Kesho Alhamisi au Ijumaa atawasili nchini kwa ajili ya Kuanza maandalizi ya Msimu Mpya na Klabu yake mpya ya Azam FC .