Arthur Bada mbioni kutua JS Kabylie


Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Singida Black Stars, Arthur Bada, ambae alikuwa na msimu bora sana katika Klabu ya Singida Black Stars, yupo katika hatua nzuri za kujiunga na Klabu ya JS KABYLYE ya Algeria akitokea Singida Black Stars.

Mpaka sasa Klabu ya JS Kabylye na Singida Black Stars wapo hatua nzuri za kufanya biashara ya Kiungo Bada kwani tayari vitu vya mhimu na maridhiano mhimu yamefanyika.

Awali Yanga SC walimwitaji Nyota huyo lakini mambo yamekwenda sio kwani yanga wamepata Kiungo mwingine ambae atazima katikati na Aucho.