Viongozi wa Yanga SC ni vidume kweli kweli


Ameandika Prince Deogratius Mchambuzi wa Soka Sports

Kuna wakati unawaza hawa viongozi wa Yanga SC ule msimamo wao wa Hatuchezi na tupo tayari kwa lolote waliutoa wapi?

Lakini unapata picha ya kuwa hawa ni viongozi waliojitoa muhanga kweli kweli kuhusu maendeleo ya mpira wetu wa Tanzania,

Kwa kashkash ambazo wamewapa TFF na bodi ya ligi kuu ya NBC

Naimani hizo taasisi zimepata elimu kubwa sana kutoka kwa Yanga SC na muda sio mrefu tutaona mabadiliko makubwa sana kwenye ligi yetu

Na huu utakuwa ni wakati mzuri wa TFF na bodi ya ligi kuu ya NBC kusahihisha makosa yao na kuja na mikakati mipya zaidi,

Hakika Yanga SC wamewashikisha adabu hao viongozi wa TFF na bodi ya ligi kuu ya NBC,

Wamshukuru sana Raisi wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN

Tofauti na hapo, Yanga SC ilikuwa inaondoka na watu pale TFF na bodi ya ligi kuu ya NBC,

Hali ilikuwa ni mbaya sana, lakini Mama katuliza upepo dakika za mwisho kabisa,

Hawa viongozi ni mfano mzuri wa kuigwa na hakika watakumbukwa sana kwenye ramani ya mpira wa Tanzania.