Inasemekana kuwa kambi ya klabu ya Simba kuelekea mchezo wa dabi ilivunjwa ikiwa ni ishara ya kutopeleka timu June 25, lakini mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu aliamuru klabu ifanye maandalizi ya mwisho ikashiriki mchezo huo pasipo kufanya mazungumzo ya kina na viongozi wengine wa klabu hiyo.
Hapa ndipo inaponukuliwa kauli ya kocha Fadlu, kuwa mambo yaliharibika kuanzia nje ya uwanja na sababu kubwa ni uongozi wa klabu hiyo maanake hata wachezaji hawakuwa psychologically wala physically fit kuelekea mchezo huo.
NB: Ubora wa taasisi au hata kampuni unategemea uimara na muunganiko mzuri wa viongozi wa taasisi husika hata nyumbani wazazi wasiposimama imara basi familia lazima
iyumbe.