Simba yakubali yaishe, kucheza dabi tar 25, Juni kwa Mkapa


Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu ameweka wazi rasmi kuwa klabu hiyo itashiriki kikamilifu kwenye mchezo wa kiporo namba 184 uliopangwa kuchezwa tarehe 25/06/2025 katika dimba la Benjamin Mkapa,

Murtaza Mangungu pia ameweka sawa na kukanusha tetesi zinazodai ndani ya klabu Kuna mivutano,amesema kuwa hakuna mgogoro wowote uliopo baina ya wanachama na Bodi ya wadhamini,wote wapo pamoja kukamilisha msimu huu unapenda kutamatika hivi karibuni.