Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya
"Mpango wa Nyuma Mwiko kushinikiza Katibu Mkuu wa TFF na Mtendaji wa Bodi ya Ligi wajiuzulu ni mpango wa makusudi wa kutaka kuweka watendaji wapya katika taasisi hizo watakaolinda maslahi yao na kuwapendelea wao
Pia kutaka kuvunjwa kwa kamati ya uendeshaji ya Bodi ya Ligi ni mkakati wa makusudi wa kutaka kuunda kamati ambayo itakua chini yao kimaamuzi
Kumbuka hawa ndio Wavunjaji wakubwa wa kanuni, ikiwemo kupita Geti lisilo rasmi, viongozi wao kuvamia Pitch, Sasa wanataka kuweka kamati ambayo itafumbia macho vitendo hivyo
Kama haitoshi wanataka kuweka Watendaji wapya wa TFF na Bodi ya Ligi ambao watakua waoga kimaamuzi maana wataamini kuwa Nyuma Mwiko wakichachamaa watanin'goa madarakani hivyo watafanya kila jambo kuwafurahisha
Ndugu zetu wa Songesha mlipolala nyie ndio tumeamkia sisi kwa kiufupi ni sisi tupo mbele ya muda
Hatuwezi kuruhusu uhuni huu ufanyike, tutakula na nyie sahani moja kukomesha utoto kwenye mambo ya msingi.
Bodi ya Ligi ni chombo cha vilabu vyote hivyo hatuwezi kuachia timu moja ifanye maamuzi kwa ajili ya wengine wengi na sisi ni Wanachama wa TFF hatuwezi kuruhusu."