Rais wa LaLiga Javier Tebas ameendelea kukosoa muundo mpya wa michuanoa ya kombe la dunia la vilabu huku akisisitiza kuwa michuano hiyo ipo kwaajili ya kuharibu kalenda ya soka na kutaka iondolewe kabla ya msimu ujao wa 2029
Tebas wiki iliyopita alisema michuano hiyo ni ya kipuuzi huku akiulinganisha mchezo wa Chelsea 2-0 dhidi ya LAFC ni kama mchezo wa kurafiki kutokana na ushindani waliouonesha huku akihitaji michuano hiyo irejee katika muundo wa awali ili kuimarisha afya ya mchezo wa mpira wa miguu