Mwisho wa Wallace Karia, TFF umefika- Kiemba


Mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba, Amri Kiemba, ameweka wazi maoni yake kuhusu uongozi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, akieleza kuwa huu ndio wakati muafaka kwake kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wapya kuendeleza mchezo huo.

“Kwa mtazamo wangu, huu ni wakati sahihi kwa kiongozi aliyeko madarakani kama Karia kutofikiria kuendelea. Kwa sababu tayari ameshakamilisha mengi na anastahili kupumzika kwa heshima. Hili ni jambo la busara sana kwa kiongozi yeyote ambaye ameshatumikia kwa muda mrefu,”- Amri Kiemba.