Menejimenti ya Edwin Balua yakana ulevi kwa mteja wao

Kampuni inayo msimamia mchezaji Edwin Balua imetoa taarifa kwa umma inayosema

"Tumeona taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mchezaji wetu Edwin Charles Balua kuhusishwa na matumizi ya vilevi, tunapenda kuliweka wazi kwa wapenzi na mashabiki wa Edwin Balua kwamba, mchezaji hajawahi kutumia wala hatumii kilevi cha aina yoyote kile.

Sambamba na hilo, timu anayoitumikia ina utaratibu wakupima wachezaji wake mara kwa mara, na katika vipindi hivyo vyote, hajawahi kukutwa na matumizi ya vilevi.

Kutokupata nafasi ya kucheza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, hakuna uhusiano wowote na matumizi ya vilevi, bali, ni mipango ya benchi la ufundi kumpa nafasi mchezaji wanayeona ameonyesha kitu kikubwa mazoezini na wanayeamini atasaidia timu katika mashindano husika kutokana na mahitaji ya timu katika mechi inayowakabili.

Tunatoa rai kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutafiti taarifa na kutoa taarifa kamili kwa umma bila kuwa na mkanganyiko wa aina yoyote ile ili kulinda heshima, na jina la mchezaji.

Imetolewa na Menejimenti

Wild & Soccer Pro Ltd