Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Clatous Chota Chama anamaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na mabingwa wa nchi na hakuna mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba.
Inasemekana baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu bara dhidi ya waajiri wake wa zamani Simba SC na mchezo wa fainali ya kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars kiungo huyo raia wa Zambia anaondoka rasmi kikosini hapo.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani Blog inapenyezewa kwamba kuna timu moja nje ya Tanzania imetuma ofa kwake na atatimkia huko Ili kujiunga nayo.
Kwaheri Mwamba wa Lusaka, Triple C.