Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kisocky amewataka wadau wa soka kuheshimu kanuni na sheria za mchezo huo Ili kuendesha vema.
Hayo ameyasema leo alipokuwa anazungumza na kipindi cha michezo cha Radio One cha saa 9 alasiri ambapo amedai kwamba viongozi wa soka hasa wa Shirikisho au vilabu ni wahanga wakubwa katika matumizi ya Sheria na kanuni.
Kisocky amewasisitiza sana kutokana na sakata lililogubika sana la klabu ya Yanga na TFF na Bodi ya Ligi lililochukua sura kiasi kwamba Rais wa nchi mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati.