Hatimaye Kasongo na Mnguto nje Bodi ya Ligi

Rasmi sasa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mnguto na CEO wa Bodi hiyo ya Ligi Almas Kasongo wameondoshwa na kupisha dabi ya Yanga na Simba Juni 25.

Yanga SC iligomea kucheza dabi ya Juni 15 ikitaka CEO wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo ajiuzuru huku pia ikimtaka mwenyekiti wa Bodi hiyo Stephen Mnguto naye ajiuzuru.

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kusuluhisha mgogoro wa Yanga na TFF na Bodi ya Ligi na hatimaye dabi sasa itapigwa Juni 25.

Viongozi wawili wa Bodi hiyo ya Ligi Kasongo na Mnguto mmoja akijiuzuru na mwingine akisimamishwa, huku bado katibu wa TFF akisubiliwa kubwaga manyanga.