Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, ameachiwa kwa dhamana leo baada ya kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kufuatia wito wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, mahojiano hayo yalitokana na malalamiko yaliyowasilishwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, akimtuhumu Manara kwa kuandika kupitia mitandao ya kijamii kwa kumtaka ajiuzulu, akidai kuwa TFF inadaiwa na Klabu ya Yanga.
Hata hivyo, Manara amekanusha tuhuma hizo, akisisitiza kuwa hajawahi kutoa taarifa hizo kama inavyodaiwa.
Baada ya mahojiano, Manara aliachiwa kwa dhamana huku uchunguzi wa suala hilo ukiendelea.