Esperance yaanza vibaya kombe la Dunia la vilabu

WAWAKILISHI wa Afrika, Espérance ya Tunisia wameanza vibaya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya kufungwa mabao 2-0 na Flamengo ya Brazil katika mchezo wa KUndi D usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Marekani.

Mabao ya Flamengo yamefungwa na mawinga wa Uruguay, De Arrascaeta dakika ya 17 na Luiz Araújo wa Brazil dakika ya 70 mbele ya mashabiki 25,797 waliojitokeza katika mechi iliyochezeshwa na refa Mholanzi, Danny Makkelie.

Mchezo mwingine wa Kundi D jana usiku Chelsea ya England ilianza vyema kwa ushindi wa 2–0 dhidi ya wenyeji, Los Angeles FC mabao ya winga Mreno, Neto dakika ya 34 na kiungo Muargentina, Enzo Fernández dakika ya 79 Uwanja wa Mercedes-Benz Stadium, Atlanta mechi iliyochezeshwa na refa Jesús Valenzuela wa Venezuela.