Azam FC yaanza na Malima wa Zed FC ya Misri

Azam FC imekamilisha rasmi usajili wa kiungo fundi Muhsin Malima kutoka klabu ya Zed FC ya nchini Misri

Malima amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza muda, akitarajiwa kuimarisha safu ya kiungo cha kati ya Wanalambalamba kwa msimu wa 2025/26.

Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam katika dirisha hili la usajili, akifuata nyayo za mlinda mlango mahiri Aishi Manula aliyesajiliwa kutoka Simba SC.

Kabla ya safari ya Misri, Malima aling'ara akiwa na Dodoma Jiji FC na sasa anarudi nyumbani kuonyesha kiwango kilichompeleka nje ya nchi.

Azam FC wameamua kuanza haraka, ni wazi dirisha hili litakuwa moto