Klabu Yetu Ilipigania Uhuru Wa Nchi Kwa Mara Nyingine Imepigania Ukombozi Wa Mpira - Simon Patrick
Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa aliyekuwa Mkurugenzi wa sheria wa Yanga SC Simon Patrick ameandika
"Klabu kubwa ilipigania uhuru wa nchi hii, kwa mara nyingine imepigania ukombozi wa mpira wa miguu wa Tanzania.
Niliwahi kusema ukombozi wa mpira wa Tanzania hauko mbali, hatimae muda umeongea.
Hongera sana Rais, Kamati ya Utendaji, Sekretariat, Wanachama na Mashabiki wa Yanga, hili ni jambo kubwa kwa mpira wa miguu wa Tanzania. Sasa kipigwe!".