Wakati aliyekuwa kaimu wa mkurugenzi wa Taifa, Ally Mayai Tembele akitarajia kurudisha fomu kwenye ofisi za TFF akiwa ni mgombea wa nafasi ya Urais, imebainika kwamba anakatwa na jina pekee la Urais litabaki moja ambalo ni la Wallace Karia.
Kukatwa kwa jina la Mayai ni kwamba amekosa vigezo vinavyomfanye awe mgombea wa nafasi hiyo hivyo sasa Karia atakuwa mgombea pekee.
Mayai amekosa wadhamini (Indosment) ambapo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, wadhamini wanatakiwa wawe 46 na tayari wadhamini wote wamemdhamini mgombea mmoja ambaye ni Karia.
Kukatwa kwa Mayai kuko kisheria kwani katiba ya TFF kuhusu uchaguzi inasema hivyo, Mayai ambaye aliwahi kugombea Urais, alikuwa nahodha wa zamani wa Yanga SC, pia amewahi kucheza timu ya taifa, Taifa Stars na CDA ya Dodoma.