Afrika Kusini yatinga fainali COSAFA

WENYEJI, Afrika Kusini wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Comoro katika mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Uwanja wa Toyota, Free State Jijini Bloemfontein nchini Afrika Kusini.

Mabao ya Bafana Bafana yamefungwa na Idris Mohamed aliyejifunga dakika ya nane, Boitumelo Radiopane dakika ya 14 na Kamogelo Sebelebele dakika ya 60, wakati bao pekee la Comoro limefungwa na Ibrahim Madi dakika ya 29.

Sasa Bafana Bafana itakutana na mabingwa watetezi, Angola ‘Palancas Negras’ ambao mapema jioni ya leo wameichapa Madagascar 4-1 hapo hapo Uwanja wa Toyota.