Yanga sasa haina majeruhi


Kuelekea Mchezo wao Ujao April 07 dhidi ya klab ya Coastal Union, Kikosi cha Young Africans Leo jioni Kiliendelea na mazoezi katika dimba la Kmc,

Hakuna majeruhi kwasasa : Kiungo Khalid Aucho aliyepata majeraha akiwa na timu yake ya Taifa ya Uganda tayari ameshapona na ameonekana kufanya mazoezi kwa ukamilifu,

Yao na Azi Ki : Nao pia ni sehemu wachezaji waliofanya mazoezi kiukamilifu, Aziz ki alikuwa nje ya Uwanja kutokana na Kusumbiliwa na Nyonga huku Mlinzi wao wa kulia Yao Kouassi yeye alikuwa nje ya Uwanja akiuguza jeraha lake la goti , wote wamepona na wamerejea mazoezini,

Chama na Musonda : Wamemaliza majukumu ya Timu yao ya Taifa ya Zambia na wameshajiunga na wenzao mazoezini kuelekea mchezo ujao dhidi ya Coastal Union.