Klabu ya Yanga imeamua kufanya biashara mwisho wa msimu huu kwa kumruhusu Stefane Aziz Ki kuondoka Klabuni hapo.
.
Aziz Ki ambaye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mnono kuliko wote Afrika Mashariki na kati Kongwe(Mil 55 takribani) alisaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu mapema msimu huu.
.
Master Ki aliyekua bora sana msimu uliopita, amekua na kiwango cha panda shuka msimu huu huku wengi wakihusisha na mambo mengi ya nje ya uwanja.
.
Inasemekana Yanga wanataka kufanya biashara mapema katika kipindi ambacho nyota huyo bado hajaipoteza thamani yake kwa kiasi kikubwa kwani huenda baadae wasiambulie chochote kitu katika kuondoka kwake.