Singida Black Stars imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichabanga timu ya Fountain Gate mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu bara.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na nyota kutoka Ghana, mshambuliaji Jonathan Sowah dakika ya 30, beki Kwabena Frank Assinki dakika ya 56 na kiungo, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya 71.