Timu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida jioni ya leo imewazamisha matajiri wa Dar es Salaam Azam FC bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
Bao pekee lililowapa alama tatu Singida Black Stars limefungwa na Elvis Rupia ambaye amefikisha mabao 10 na anazidi kufukuzia kiatu cha dhahabu.
Kwa matokeo hayo sasa Azam FC haitaweza kuifikia Simba iliyo kwenye nafasi ya pili kwani pointi zake 57 hazitaweza kufikiwa na Azam.