Simba wasitegemee miujiza

Mwanahabari mkongwe wa michezo hapa nchini Prince Hoza amedai kwamba Ili timu ya Simba SC iweze kufuzu nusu fainali kwa kuitoa mashindanoni Al Masry inahitaji kujitoa vya kutosha na isitegemee miujiza.

Hoza ambaye anaandikia gazeti la MSIMBAZI, amesema leo jijini Dar es Salaam kwamba Wanasimba wanaamini kwamba timu yao itaibuka na ushindi na kuitupa nje Al Masry.

"Simba inatakiwa kushinda magoli 3-0 baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza ugenini, nimewaangalia Simba wamecheza vizuri ila walizidiwa mbinu na ndio maana wakafungwa", alisema na kuongeza.

"Wale jamaa ni wazuri na wala Simba wasitegemee miujiza kwamba inaweza kuwafunga kama walivyowafunga Horoya au Jwaneng, Al Masry ni timu kubwa na ina uzoefu hivyo Simba wategemee uwezo wao na sio maajabu.

Aliendelea kusema mwanahabari huyo ambaye pia anachambua kwenye vituo kadhaa vya redio hapa nchini, Hoza anasema Simba inatakiwa kutinga nusu fainali na kuondoa dhana ya kuishia robo fainali.

Simba na Al Masry zitarudiana Aprili 9 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, kila la kheri Simba SC

Prince Hoza mchambuzi wa soka