Wenyeji Al Masry usiku huu wameanza vema mkondo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Simba SC mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga mabao 2-0 uwanja wa New Suez canal Misri.
Dakika ya 16 Abderrahim Deghmoum aliipatia Al Masry bao la kuongoza kabla ya kipindi cha pili dakika ya 89 Jony Ebuka kufunga la pili na kuhitimisha kwa ushindi huo.
Timu hizo zitarudiana tena jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa Aprili 9 ambapo Simba inatakiwa kushinda mabao 3-0 Ili kusonga mbele
.