Mashujaa FC yaifumua Fountain Gate

Timu ya Mashujaa FC ya Kigoma imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Lake Tanganyika.

Mabao ya Mashujaa FC yamewekwa kimiani na Jaffary Kibaya dakika ya 32, Idrissa Stambuli dakika ya 48 na Seifu Karihe dakika ya 77, huo ni mwanzo mzuri wa kocha wao mpya Salum Mayanga aliyechukua mikoba ya Mohamed Abdallah Baresi.