Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini Burundi (FFB )Jeremie Manirakiza anadaiwa kukamatwa baada ya kurejea kutoka katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 wiki iliyopita.
Katika mechi za kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia hivi karibuni Burundi ilipoteza baada ya kufungwa na Ivory Coast bao 1-0 na baada kupata ushindi mnono dhidi ya Shelisheli wa 5-0.
Hadi kufikia sasa hazijajulikana sababu za kukamatwa kwake.