JKT Tanzania yaibugiza Dodoma Jiji 2-1

Timu ya JKT Tanzania imeifunga Dodoma Jiji mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Meja Isamuyo uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mabao ya JKT Tanzania yote yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Edward Songo dakika ya 25 kwa penalti na dakika ya 67, wakati ya Dodoma Jiji yamefungwa na kiungo Mwana Kibuta David dakika ya 45'+2 na mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 81.