Siku chache baada ya kocha mkuu wa Orlando Pirates, Jose Reveiro kuwaambiwa waajiri wake hana mpango wa kuongeza mkataba mpya, bali ifikapo mwishoni mwa msimu anaondoka kikosini hapo, tayari uongozi umeingia mawindoni kutafuta mbadala wake.
Miongoni mwa wakufunzi hao wanaofuatiliwa kwa karibu sana kupata saini yake ni Davids Fadlu kutoka Simba kumrejesha ardhi ya nyumbani Afrika Kusini.
Orodha hiyo wamo Wasauzi wengine wawili,Pitso Mosimane aliyepo kwa sasa Falme za Kiarabu pamoja na Rhulani Mokwena kutoka Wydad Casablanca(Morocco).