Elvis Rupia kwenye msimu mzuri na mabao yake 9

Mshambuliaji wa Singida Black Stars raia wa Kenya, Elvis Rupia amekuwa katika kiwango bora msimu huu baada ya kufunga mabao tisa ya Ligi Kuu Bara hadi sasa, ikiwa ni idadi kubwa kwa nyota huyo tangu aanze kucheza soka hapa nchini.

Rupia alijiunga na kikosi hicho msimu wa 2023-2024 akitokea Police FC ya kwao Kenya na alifunga mabao 27 na kuivunja rekodi iliyochukua miaka 47, katika Ligi Kuu ya Kenya ya Moris Aloo Sonyi aliyefunga 26, mwaka 1976, akiwa na Gor Mahia.

Katika msimu wake wa kwanza, Rupia alichezea timu mbili tofauti akianzia Singida Fountain Gate kisha dirisha dogo akatua Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars na kwa msimu mzima alifunga jumla ya mabao sita akiwa na klabu zote mbili.