Mshambuliaji Shabani Iddi Chilunda ameiongoza KMC katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Shaaban Chilunda mawili dakika ya 42 kwa penalti na 67 na Msomali, Ibrahim Elias dakika ya 55, wakati ya Tanzania Prisons yote yamefungwa na Haroun Chanongo dakika ya 64 na 83.