CCM Mkwakwani sasa ruksa

Shirikisho la soka nchini, TFF limeuruhusu uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga kutumika kwa mechi za Ligi Kuu bara zilizobakia msimu huu.

Uwanja wa CCM Mkwakwani unatumiwa na timu ya Coastal Union kama uwanja wake wa nyumbani sasa utatumiwa kwenye mechi zote ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji.

Coastal Union ilikuwa ikiutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kama uwanja wa nyumbani lakini pia iliwahi kuutumia uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.