Kocha wa zamani wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema kwamba aliwaambia Simba wawe makini kwenye Idara ya ulinzi wanapocheza na Al Masry lakini hawakumsikia.
Hayo ameyadai baada ya kufungwa mabao 2-0 na kufifisha matumaini yao ya kutinga nusu fainali.
"Nilishawaambia hawa Simba kuweni makini sana kwenye safu yenu ya ulinzi maana hawa Al Masry wana washambuliaji hatari hawakunielewa mmeona
kilichotokea? Alilalamika Benchikha.