Andiko la Haji Manara kwa RC wa mkoa wa Tabora


Kwako RC wa Mkoa wa Tabora

Salaam Mhe. Paul Chacha

Nimekaa kwenye Mpira kwa muda mrefu kidogo na pengine mimi ndio Binadaam pekee niliyewahi kuhudumu kuwa Msemaji wa hivi Vilabu vyetu vikubwa nchini.

Najua nguvu ya hizi Taasisi hususan kwenye eneo la ushabiki,Naelewa pia unakuwa katika hali gani unapokuwa unazungumzia hizi team.

Na najua pia kazi yenu ya kuhamasisha Michezo kwenye mikoa mnayoiongoza,Sometimes tunakuwa excited na kama Binadaam tunaweza kupitiliza.

Lakini we ni kiongozi mkubwa,Naomba endelea kuwa na ngozi mgumu,Uongozi ni pamoja na kubeba kila kitu,
Rudisha Moyo wako nyuma, kijana huyu ni sawa na mwanao au mdogo wako wa mbali mno.

Naelewa kwa nafasi yako ukiwa mkoani kwako unahitaji heshma na kwa rika lako ni rahisi kutambua situation zetu za mambo ya kimpira!!

Mimi kama kaka Mkubwa wa hawa wadogo zetu nikuombe sana tusonge mbele Mkuu.

Na sitaki kwenye barua hii kusema chochote katika kutafuta mkosaji lakini kwako kama Mkubwa tunakuomba limalize hili na kwa dhati nikuombe ulipokwazika samehe.
Sisi bado tunaendelea kujifunza na kwenye kujifunza may be tunaweza kuteleza.

"hajawa mjinga yule ajishushae kwa Mkubwa, kusema samahani hata kwa kile unachoona upo sahihi" Jimmy Carter 2/8/1987