Alikamwe alivuka mipaka- Kamanda wa Polisi Tabora

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Richard George Abwao amewataka wanamichezo kutopenda kutoa matamko yanayovuka mipaka hasa kwa wenye mamlaka.

"Alikamwe hili ni kosa ambalo amelifanya na amelifanya dhidi ya Kiongozi, linaweza kuwa na athari kubwa, na ukiangalia hata kwenye maneno ambayo ameyatamka anatamka kama kwenda kuitaja au kama kwenda kuisemea mamlaka ya uteuzi ambayo inamhusu kiongozi mkubwa hili ni kosa"

"Unapozungumzia mambo ya kimichezo yazungumziwe kwenye mipaka ya mambo ya kimichezo, lakini mambo mengine ambayo yanahusu heshima na hadhi za viongozi yanatakiwa kubaki kwenye msitari wake"Amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard George Abwao, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo.