Zamalek yapewa pointi 3 na magoli 3 Al Ahly kususia mchezo

Baada ya Al Ahly kugomea dabi ya Cairo, Zamalek imechukua ushindi wa mezani wa mabao 3-0 pamoja na pointi tatu ambapo uamuzi huu umefuata kanuni za ligi ambazo zinatoa ushindi kwa timu iliyofika uwanjani ikiwa mpinzani wake hajajitokeza bila sababu inayokubalika.

Al Ahly walibaki na msimamo wao wa kutaka Waamuzi wa kigeni pekee kuendesha mchezo huo lakini Waamuzi wa ndani walioteuliwa waliwasili uwanjani na kutangaza kumalizika kwa mechi baada ya kutokuwepo kwa Al Ahly.

Mpaka sasa Al Ahly hawajatoa tamko jipya kuhusu hatua hii huku Mashabiki na wadau wa soka wakisubiri iwapo klabu hiyo itachukua hatua zaidi dhidi ya uamuzi huo.