Timu ya Yanga Princess imetinga hatua ya fainali ya kombe la Samia Super Cup baada ya kuifunga bila huruma timu ya Fountain Gate mabao 7-0 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Kwa ushindi mkubwa, Yanga Princess imetinga fainali na itakutana na JKT Queens ambayo leo imewaondoa Simba Queens kwa kuilaza bao 1-0 katika uwanja huo huo.
Fainali itachezwa Machi 6 na bingwa ataandika historia ya kuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo.