Aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sanaa na Utamaduni (Michezo) Profesa Philemon Mikoi Sarungi amefariki dunia.
Sarungi ambaye alikuwa Mbunge wa kuchaguliwa Jimbo la Rorya mkoani Mara, alikuwa shabiki kindakindaki na mwanachama wa Simba SC ambapo nao wametuma salamu za rambirambi.
"Tumesikitishwa na kifo cha babu yetu, aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo letu la Rorya, Waziri na daktari bingwa Profesa Philemon Mikol Sarungi kilichotokea leo jioni.
Tunaungana na wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kufarijiana katika kipindi hiki kigumu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe wote tuseme R.I.P Babu yetu Sarungi, waliandika wana Rorya kupitia ukurasa wake wa wana Rorya.