Timu ya Wanawake ya Al Nassr imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Saudi Arabia wakiwa na michezo miwili mkononi.
Timu hiyo anayokipiga nyota wa Tanzania, Clara Luvanga imetwaa ubingwa huo baada ya kufikisha alama 48 katika mechi 16 walizocheza, wakipata ushindi mechi mechi zote 16 wakifunga jumla ya mabao 62 na kuruhusu kufungwa mabao 14.
Al-Nassr imetwaa ubingwa huo kwa misimu tatu mfululizo 2022-23, 2023-24 na sasa 2024-25.
Ligi Kuu ya Wanawake ya Saudi Arabia (Saudi Women's Premier League) ilianza kutimua vumbi rasmi mwaka 2022, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza soka la wanawake nchini Saudi Arabia.