TFF yaufungulia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uwanja huu ulifungiwa kutokana na miundombinu kutokidhi vigezo tofauti na kanuni ya leseni za Klabu. TFF wametoa nafasi kwa timu zote zilizokuwa zinatumia Uwanja huu kwa michezo ya nyumbani kuendelea kuutumia kuanzia sasa.