Shirikisho la soka nchini, TFF limefungia viwanja vitatu kuendelea kutumika kwaajili ya michezo ya Ligi Kuu bara.
Viwanja vilivyofungiwa kutokana na miundombinu yake kuchakaa ni pamoja na uwanja wa Liti mjini Singida, CCM Kirumba Mwanza na Jamhuri mjini Dodoma.
TFF tayari ilishaufungia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na sasa timu za Dodoma Jiji inayotumia uwanja wa Jamhuri, Singida Black Stars inayotumia uwanja wa Liti na Pamba Jiji inayotumia uwanja wa CCM Kirumba kutafuta viwanja vingine.