Baada ya kuigomea Yanga SC Jumamosi iliyopita, jioni ya leo katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam, Simba SC imeishushia kipigo cha mabao 3-0 na kutinga hatua ya 16 bora kombe la CRDB Cup.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na beki Mburkinabe, Valentin Nouma dakika ya 17, mshambuliaji Sixtus Robert Sabilo aliyejifunga dakika ya 19 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida dakika ya 76.
Wakati huo huo michuano hiyo iliendelea kwa timu ya Kiluvya United ikiikaribisha Pamba Jiji na Pamba kushinda 3-0 wakati Kagera Sugar ikiikaribisha Namungo FC na Kagera kushinda pia 3-0