Mchambuzi wa Michezo wa Wasafi Fm (Ricardo Momo) amesema kuwa kitendo cha Klabu ya Simba kugoma kucheza mechi yake dhidi ya Yanga ni mpango ambao waliupanga muda mrefu kwasababu wachezaji wao muhimu hawapo timamu kimwili hivyo ingekuwa rahisi sana kwa wao kupoteza hiyo mechi
Momo amesema kwamba Simba wanajua ile ndio mechi muhimu zaidi iliyobaki yenye kuamua hatima yao ya Kugombania ubingwa hivyo wasingeweza kucheza kucheza ikiwa wachezaji wao hawapo timamu kushindana na Yanga.
Pia momo amegusia hata kitendo cha SIMBA kupeleka timu usiku kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi bila kutoa taarifa kwa wahusika ni mpango wao kwasababu walijua hawatoruhusiwa kuingia hivyo wakatumia plan hiyo ili kutokee vurugu wapate sababu ya kutocheza.