Simba na Dodoma Jiji sasa ni Machi 14

Hatimaye kile kiporo kati ya Simba SC na Dodoma Jiji kimepangiwa tarehe na sasa timu hizo zitakutana Machi 14, 2025 katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo imesogezwa mbele kwa sababu iliahirishwa baada ya wachezaji wa Dodoma Jiji walipata ajali hivyo Bodi ya Ligi iliifuta mechi hiyo.