Simba kuhamia Rwanda au Uganda

Inasemekana klabu ya Simba inaweza kuhamia uwanja wa Amahoro nchini Rwanda au Nelson Mandela Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masr ya Misri.

Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambao Simba imekuwa iloutumia kama uwanja wa nyumbani umezuiwa na CAF na imejulishwa kutafuta uwanja mwingine.

Duru za kispoti zinasema kwamba Simba inahamia Amahoro au Mandela kwani miundombinu yake Iko vizuri.