Taarifa kutoka nchini Morocco zinaeleza kwamba nyota wa kimataifa wa Tanzania, Selemani Mwalimu ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa mbele.
Mwalimu amekuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili sasa kutokana na kupata maumivu ya paja.
Hata hivyo leo klabu ya Wydad Casablanca imetoa kikosi kitakachoivaa FUS Rabat hapo kesho kwenye muendelezo wa ligi kuu Botola.
Kikosi cha wachezaji 23 jina la Selemani Mwalimu halipo, kutokana na kuwa majerehu kwa wiki kadhaa sasa.