Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne Samuel Eto’o ameshinda haki ya kujumuishwa kwenye orodha ya wagombea wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Afrika CAF.
Hakuna sababu zilizotolewa wakati CAF ilipomtenga Eto'o mwezi Januari.
CAF wiki ijayo itafanya uchaguzi wa nyadhifa zake za juu, ikiwa ni pamoja na Rais wa shirikisho na wawakilishi wa bara kwenye Baraza la FIFA.