Kocha Salum Mayanga amejiunga na Mashujaa FC akitokea Mbeya City ya NBC Championship.
Salum Mayanga msimu huu akiwa na Mbeya City ameingia robo fainali ya Kombe la shirikisho la CRDB na pia yupo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Championship akiwa na alama 49.
Mashujaa FC muda sio mrefu watamtangaza Mayanga ambae anachukua nafasi ya Mohammed Bares na ataanza kazi yake mpya ndani ya Mashujaa FC.